Sisi ni Nani?

Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) ni Taasisi ya Serikali chini ya Wizara ya Kilimo. NFRA ilianzishwa chini ya Sheria ya Wakala Na. 30 ya mwaka 1997. Hati ya kuanzisha rasmi Wakala ilitolewa kwa Tangazo la Serikali Na. 81 lililochapishwa tarehe 13 Juni 2008 na kuanza kazi rasmi tarehe 1 Julai, 2008. Hati hiyo ilihuishwa kwa Tangazo la Serikali Na. 120 lililochapishwa tarehe 15 Aprili 2016.