Majukumu
Ili kufikia dira na dhima, Wakala unatekeleza majukumu yafuatayo:-
i. Kuhifadhi akiba ya chakula toshelevu kwa mahitaji ya nchi;
ii. Kununua, kuhifadhi na kutoa akiba ya chakula ili kukabiliana na majanga;
iii. Kuzungusha na kutafuta masoko ya chakula ili kupunguza mfumuko wa bei na kuingiza mapato;na
iv. Kutoa huduma mbalimbali za uhifadhi ili kuongeza mapato.
Katika kutekeleza majukumu hayo, Wakala huweza kutumia vyanzo vifuatavyo vya Mapato:
i. Ruzuku kutoka Serikalini;
ii. Mauzo ya akiba ya chakula;
iii. Fedha zinazopatikana kutokana na huduma zinazotolewa na Wakala;
iv. Mikopo kutoka taasisi za fedha;
v. Misaada kutoka kwa washirika wa maendeleo.