Kanda ya Songwe

Ofisi za Kanda ya Songwe zipo katika eneo la Mbozi, Mkoa wa Songwe na inaongozwa na Meneja wa Kanda. Kanda ilianzishwa ili kuhudimia Mikoa wa Songwe na Mbeya kutokana na uzalishaji mkubwa wa ziada ya nafaka hususan mahindi na mpunga, na kuweza kuhudumia Kanda zingine za Wakala zenye uzalishaji mdogo. Kanda ya Songwe ina maghala yenye uwezo wa kuhifadhi tani 17,000 za nafaka.

Kwa sasa, Wakala inatekeleza mradi wa kuongeza uwezo wa kuhifadhi nafaka kwa kujenga vihenge na maghala ya kisasa ili kuboresha miundo ya uhifadhi katika eneo la Vwawa. Kukamilika kwa mradi huu kutawezesha kuongeza uwezo wa kuhifadhi nafaka kutoka tani 17,000 zilizopo sasa hadi tani 37,000.

Nafaka zinazonunuliwa, kuhifadhiwa na kuzungushwa/kuuzwa kupitia Kanda ya Songwe ni mahindi na mpunga.

Mawasiliano;