Changamoto

CHANGAMOTO ZINAZOIKABILI WAKALA WA TAIFA WA HIFADHI YA CHAKULA

Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya chakula inakabiliwa na Changamoto kuu tatu:

  1. Uweza wa kuhifadhi.
  2. Mifumo hafifu wa Tathimini na Ufuatiliaji.
  3. Utumiaji wa Teknologia iliyopitwa na wakati.

Wakala umepanga kutekeleza mikakati ifuatayo ili kukabiliana na changamoto unazoukabili

(i) Kuongeza uwezo wa uhifadhi kutoka tani 246,000 za sasa hadi kufikia malengo ya tani 450,000 ifikapo 2017/2018. Malengo haya yatafikiwa kupitia utekelezaji wa mradi kwa kutumia fedha za mkopo wa masharti nafuu kutoka Serikali ya Poland. Aidha, Wakala unaendelea kufanya majadiliano na taasisi za fedha za ndani na nje ya nchi pamoja na wawekezaji binafsi ili kupata fedha zaidi zitakazowezesha kutekeleza mipango ya maendeleo ya Wakala ikiwa ni pamoja na azma ya Serikali ya kuongeza uwezo wa kuhifadhi nafaka hadi kufikia tani 1,000,000.

(ii) Kuboresha mifumo ya utendaji kazi ikiwemo matumizi sahihi na stahiki ya TEHAMA.

(iii) Kuwezesha Wakala kuwekeza katika teknolojia, vifaa, zana na njia za kisasa katika uhifadhi wa akiba ya chakula.

(iv) Kupanua wigo wa mapato ikiwa ni pamoja na kuchukua mikopo kutoka katika taasisi za fedha, misaada ya wahisani, kushirikiana na sekta binafsi katika kuwekeza katika miundo mbinu na teknolojia za kisasa za hifadhi.