Albamu ya Video

UWEKAJI JIWE LA MSINGI UJENZI WA MAGHALA NA VIHENGE VYA KISASA

Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Bi. Vumilia L. Zikankuba, anapenda kuutaarifu Umma wa Watanzania kwamba Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb), ataweka jiwe la msingi katika Mradi wa Ujenzi wa Vihenge na Maghala ya Kisasa. Sherehe hiyo itakayofanyika Makao Makuu ya NFRA yaliyopo Mtaa wa Kizota mjini Dodoma katika eneo la Viwanda siku ya Jumamosi tarehe 21 Aprili, 2018 saa 4.00 kamili asubuhi. WOTE MNAKARIBISHWA

Imewekwa: Apr 25, 2018

Tazama makala iliyoandaliwa na NFRA kuhusu utaratibu bora wa uvunaji na uhifadhi bora wa mahindi

Ni mategemeo ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) kwamba, kupitia Makala hii, Wakulima na wadau wengine wa mahindi wataweza kufahamu mbinu bora za uvunaji na uhifadhi wa mahindi, pamoja na kutambua vigezo vya ubora vinavyohitajika na Wakala wakati wa ununuzi, hivyo kupunguza changamoto zinazojitokeza wakati wa kutekeleza kazi ya ununuzi wa nafaka ya mahindi

Imewekwa: Sep 20, 2018

NFRA lazima inunue nafaka ya kutosha kwa niaba ya serikali Mhe Hasunga

Imewekwa: Jan 08, 2019

Mhe Hasunga aitaka TBA kusimamia kwa weledi mradi wa maghala na vihenge vya kisasa Songea

Imewekwa: Jan 08, 2019