Habari

NFRA YAPATIWA MAGHALA KUONGEZA UWEZO WA UHIFADHI WA NAFAKA

NFRA YAPATIWA MAGHALA KUONGEZA UWEZO WA UHIFADHI WA NAFAKA
Jan, 16 2024

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. David Silinde(Mb), akimkabidhi Mkurugenzi wa Huduma Saidizi wa NFRA, Bw. Mohamedi Ally, cheti cha umiliki wa Maghala ya Mradi wa kudhibiti sumu kuvu nchini TANPACK na kuwa mmiliki halali wa Maghala hayo, makabidhiano hayo yamefanyika tarehe 12 Desemba, 2023 katika kata ya Mrijo Kijiji cha Mrijo Chini Wilayani Chemba.

Naibu Waziri alielekeza NFRA kuhakikisha Maghala hayo yanatumika kulingana na mwongozo uliotolewa na wananchi wanufaike kupitia Mradi huo.