Uhifadhi

Wakala hutekeleza majukumu yake nchi nzima kupitia kanda zake saba zilizoanzishwa kimkakati ambazo ni Arusha, Kipawa, Dodoma, Shinyanga, Makambako, Sumbawanga na Songea. NFRA ina maghala 33 yenye uwezo wa kuhifadhi tani 246,000. Mgawanyo wa mikoa kikanda pamoja na uwezo wa uhifadhi kikanda umeainishwa katika jedwali hapa chini.

Kanda

Uwezo wa Hifadhi(Tani)

Mikoa Inayohudumiwa na Kanda

Arusha

39,000

Arusha, Kilimanjaro na Manyara

Kipawa

52,000

Dar es Salaam, Pwani, Tanga, Morogoro, Mtwara na Lindi

Dodoma

39,000

Dodoma na Singida

Shinyanga

14,500

Shinyanga, Tabora, Mwanza, Mara, Kagera, Geita, Simiyu na Kigoma

Makambako

39,000

Iringa, Mbeya, Njombe na Songwe

Songea

29,000

Ruvuma

Sumbawanga

38,500

Rukwa na Katavi

Jumla

251,000