Mafanikio

Wakala umefanikiwa kutekeleza majukumu yake kikamilifu na kwa ufanisi kila mwaka, baadhi ya mafanikio hayo ni pamoja na:-

Kununua mazao ya chakula cha ziada kutoka kwa wakulima: Wakala umefanikiwa kwa kiwango kikubwa kununua mahindi ya ziada kutoka kwa wakulima na kutimiza malengo yaliyowekwa na serikali kila mwaka.

Kuhifadhi akiba ya kutosha katika maghala yake: NFRA imeafanikiw akuwa na akiba ya kutosha ya chakula kila mwaka kwa ajili ya kukabiliana na majanga ya njaa kila yanapojitokeza nchini.

Kutoa Chakula cha msaada kwa waathirika: Kila inapolazimika, NFRA imekuwa ikisimamia kwa ufanisi utoaji wa chakula cha njaa kwa mamlaka za serikali za mitaa kwa kuzingatia taratibu zilizowekwa na Kitengo cha Maafa cha Ofisi ya Waziri Mkuu.

Utekelezaji wa baadhi ya mikakati iliyowekwa na Serikali: Wakala umechangia katika utekelezaji wa Mkakati wa Kukuza Uchumi na kupunguza Umaskini (MKUKUTA) kwa kutoa bei nzuri na ya kuvutia kwa wakulima wanaouza mazoa yao kwa NFRA.

Utekelezaji wa Malengo ya Milenia (2025): Wakala umechangia katika kuchochea uchumi na maendeleo ya Taifa kwa kushirikisha sekta binafsi katika kutoa huduma mbalimbali kama vile usafirishaji wa mahindi na ununuzi wa vitendea kazi kama magunia matupu