NFRA Yaendesha mafunzo kwa Watumishi wake wa Ubora
Afisa Mtendaji Mkuu NFRA akagua mradi wa kuongeza uwezo wa Uhifadhi
KAMATI YA PAC YAKAGUA UJENZI WA MRADI WA KUONGEZA UWEZO WA KUHIFADHI NAFAKA UNAOJENGWA NA NFRA
Uzinduzi wa Ujenzi wa Magala na Vihenge
Ofisi za Kanda ya Songea zipo katika eneo la Ruhuwiko, Mkoa wa Ruvuma na inaongozwa na Meneja wa Kanda. Kanda ilianzishwa kimkakati kwa kuwa Mkoa wa Ruvuma unaongoza kwa uzalishaji mkubwa wa nafaka aina ya mahindi lakini pia kuweza kuhudumia Mkoa wa Ruvuma na Kanda zingine za Wakala zenye uzalishaji mdogo wa nafaka. Kanda ya Songea ina maghala yenye uwezo wa kuhifadhi tani 29,000 za nafaka.
Kwa sasa, Wakala inatekeleza mradi wa kuongeza uwezo wa kuhifadhi nafaka kwa kujenga vihenge na maghala ya kisasa ili kuboresha miundo ya uhifadhi katika eneo la Ruhuwiko-Songea Mjini. Kukamilika kwa mradi huu kutawezesha kuongeza uwezo wa kuhifadhi nafaka kutoka tani 29,000 zilizopo sasa hadi tani 84,000.
Nafaka zinazonunuliwa, kuhifadhiwa na kuzungushwa/kuuzwa kupitia Kanda ya Songea ni mahindi. Ni kanda inayoongoza kwa kuwa na uzalishaji mkubwa wa nafaka hususan mahindi, hivyo kuwa moja ya soko linalotegemewa na Wakala katika ununuzi wa nafaka.
Mawasiliano;