Habari

NFRA YAINGIA MAKUBALIANO NA SMZ -ZANZIBAR KATIKA MAUZO YA NAFAKA

NFRA YAINGIA MAKUBALIANO NA SMZ -ZANZIBAR KATIKA MAUZO YA NAFAKA
Jan, 16 2024

Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) na Wizara ya Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (WKUMM) zimefikia makubaliano ya kuwa na ushirikiano kwenye masuala ya ununuzi/mauzo ya nafaka, uhifadhi wa akiba ya chakula, kubadilishana uzoefu na kujengeana uwezo katika masuala ya uendeshaji wa hifadhi ya chakula. Makubaliano hayo yamefikiwa tarehe 21 Desemba, 2023 ambapo Katibu Mkuu wa WKUMM Bw. Seif Shabani Mwinyi na Afisa Mtendaji Mkuu wa NFRA Dkt. Andrew Komba walisaini Randama itayoongoza utekelezaji wa makubaliano.