Uzungushaji wa Chakula

KUZUNGUSHA/KUUZA AKIBA YA CHAKULA

Katika kutekeleza majukumu yake, Wakala una jukumu la kuzungusha akiba ya chakula kwa malengo mbalimbali.

Kuzungusha/ kuuza hufanyika ili kukidhi malengo yafuatayo;

i. Kulinda ubora wa akiba ya chakula iliyohifadhiwa ghalani

ii. Kutoa nafasi ili kuhifadhi akiba mpya ya chakula,

iii. Kuongeza usambazaji wa nafaka katika masoko,

iv. Kupunguza makali ya mfumuko wa bei pale inapohitajika,

v. Kutoa huduma ya chakula kwa waathirika wa njaa, mafuriko na majanga mbalimbali kwa maelekezo maalumu ya Serikali.

vi. Kupata fedha kwa ajili ya kununua nafaka katika msimu mpya wa mavuno.



Miongoni mwa mazingira yanayosababisha uuzaji wa nafaka ni haya yafuatayo;

i. Uthibitisho wa kuwepo kwa upungufu wa chakula kwa ujumla kutokana na uzalishaji mdogo na pia katika soko kutokana na kupungua kwa uingiaji na upatikanaji wa vyakula sokoni katika baadhi ya maeneo;

ii. Kupanda kwa kasi kwa bei za soko kwa viwango vilivyo juu ya bei za wastani. Wakala hutumia bei za wastani za soko zinazotolewa na Wizara ya Viwanda na Biashara na Wizara ya Kilimo;

iii. Kuwepo kwa akiba ya kutosha ya chakula katika maghala ya Wakala inayoweza kukidhi mahitajiya chakulakwa waathirika wa upungufu wa chakula;

iv. Kuwepo kwa mahitaji ya nafaka ndani na nje ya nchi yanayotoa fursa ya kuingiza kwa mapato ya Wakala.


Njia za Kuzungusha Akiba ya Chakula

Wakala huuzanafaka kwa wadau mbalimbali kwa kuzingatia lengo la mauzo.Njia zifuatazo hutumika katika kuzungusha nafaka:

1. Kutangaza zabuni za kuuza au kushiriki katika zabuni zinazotangazwa na wadau mbalimbali wenye lengo la kununuanafaka;

2. Kuuza chakula kupitia matangazo ya wazi kwa Umma;

3. Kuuza chakula kwa taasisi mbalimbali na wadau wengine wanaobainishwa kwa kuzingatia mahitaji ya wakati ya nchi;

4. Kuuza chakula katika masoko ya nje ya nchi.

Wakala huweza kutangaza zabuni ya wazi ili kuzungusha nafaka ambapo wanunuzi wanaokidhi vigezo wanauziwa nafaka hizo. Aidha, Wakala hushiriki katika zabuni mbalimbali zinazotangazwa na wadau wengine ikiwemo Mpango wa Chakula Duniani (WFP) ili kuuza nafaka zake pale inapohitajika. Wakala pia kuzungusha nafaka kwa kuutangazia Umma kupitia vyombo vya habari kuhusu azma ya kuzungusha nafaka katika masoko wakati husika. Aidha, Wakala huweza kuzungusha nafaka kwa kuuza kwa taasisi mbalimbali za Serikali na kijamii ambazo zina mahitaji ya chakula.

PICHA: Uzungushwaji wa Chakula kupunguza makali ya bei