NFRA Yaendesha mafunzo kwa Watumishi wake wa Ubora
Afisa Mtendaji Mkuu NFRA akagua mradi wa kuongeza uwezo wa Uhifadhi
KAMATI YA PAC YAKAGUA UJENZI WA MRADI WA KUONGEZA UWEZO WA KUHIFADHI NAFAKA UNAOJENGWA NA NFRA
Uzinduzi wa Ujenzi wa Magala na Vihenge
Ofisi za Kanda ya Sumbawanga zipo katika eneo la Mazwi, Mkoa wa Rukwa na inaongozwa na Meneja wa Kanda. Kanda ilianzishwa kimkakati kutokana kuwa na uzalishaji mkubwa wa nafaka aina ya mahindi na mpunga. Kanda hii inahudumia Mkoa wa Rukwa na Katavi. Kanda ya Sumbawanga ina maghala yenye uwezo wa kuhifadhi tani 38,500 za nafaka ambapo ni Mazwi-Sumbawanga Mjini (Tani 28,500), Laela-Sumbawanga Vijijini (tani 5,000), na Mpanda-Katavi (Tani 5,000).
Kwa sasa, Wakala inatekeleza mradi wa kuongeza uwezo wa kuhifadhi nafaka kwa kujenga vihenge na maghala ya kisasa ili kuboresha miundo ya uhifadhi katika eneo la Mazwi na Mpanda. Kukamilika kwa mradi huu kutawezesha kuongeza uwezo wa kuhifadhi nafaka kutoka tani 38,500 zilizopo sasa hadi tani 83,500.
Nafaka zinazonunuliwa, kuhifadhiwa na kuzungushwa/kuuzwa kupitia Kanda ya Sumbawanga ni mahindi na mpunga. Ni moja ya kanda inayotegemewa kuhamisha nafaka kwenda kanda zenye upungufu katika uzalishaji wa chakula hususan mikoa ya kanda ya Ziwa.
Mawasiliano;