Bidhaa

Kupitia kanda zake, Wakala kwa sasa unanunua, kuhifadhi na kuuza nafaka za aina tatu;

i. Mahindi

ii. Mtama

iii. Mpunga

Nafaka hizi hununuliwa na kuuzwa katika maghala mbalimbali kwa kuzingatia upatikanaji wake. Mahindi hununuliwa na kuuzwa katika Kanda zote za Wakala. Mtama huweza kununuliwa na kuuzwa kupitia Kanda za Dodoma na Shinyanga. Aidha, mpunga huweza kununuliwa na kuuzwa kupitia kanda za Makambako, Songwe, Kipawa, Sumbawanga na Shinyanga. Nafaka hizi zinapatikana zikiwa na ubora wa hali ya juu ambao unakidhi vigezo vya ubora wa kimataifa.