Kanda ya Kipawa

Ofisi za Kanda ya Kipawa zipo katika barabara ya Mbozi, Chang’ombe Jiji la Dar es salaam na inaongozwa na Meneja wa Kanda. Kanda ilianzishwa kimkakati ili kuweza kuhudumia Mikoa ya Pwani ya mashariki ya nchi ambayo ni Dar es salaam, Lindi, Mtwara, Pwani, Tanga na Morogoro. Kanda ya Kipawa ina maghala yenye uwezo wa kuhifadhi tani 52,000 za nafaka, katika maeneo ya Chang’ombe na Kipawa.

Kanda ya Kipawa katika uanzishwaji wake ilikuwa ni mahususi kwa ajili ya kupokea akiba ya chakula kutoka katika maeneo yenye ziada ya kutosha ya uzalishaji wa nafaka. Kanda hii kimkakati ni Kanda iliyopo katika kitovu cha Jiji ambalo lina njia nyingi za upokeaji na usafirishaji wa chakula kupitia bandari za Dar es Salaam, Mtwara na Tanga, reli na barabara na pia kuwa na idadi kubwa ya watu na makazi.

Nafaka zinazonunuliwa, kuhifadhiwa na kuzungushwa/kuuzwa kupitia Kanda ya Kipawa ni mahindi,mpunga na mtama pale kunapokuwa na uzalishaji mkubwa. Mahitaji makubwa ya chakula katika Kanda hii ni kwa ajili ya kukabiliana na upungufu wa chakula katika masoko mbalimbali kutokana na Mikoa inayohudumiwa na Kanda kuwa upungufu wa mara kwa mara katika uzalishaji wa chakula na kuwa na mahitaji mkubwa ya kibiashara.

Mawasiliano;