Kanda ya Makambako

Ofisi za Kanda ya Makambako zipo katika Mji wa Makambako, Mkoa wa Njombe na inaongozwa na Meneja wa Kanda. Kanda ilianzishwa kimkakati ili kuweza kuhudumia Mikoa ya Njombe, Iringa, Mbeya na Songwe. Katika kuongeza ufanisi, Kanda hii iligawanywa na kutoa kanda mbili ambazo ni Kanda ya Makambako (Njombe na Iringa) na Songwe (Songwe na Mbeya). Kanda ya Makambako ina maghala yenye uwezo wa kuhifadhi tani 22,000 za nafaka.

Kwa sasa, Wakala inatekeleza mradi wa kuongeza uwezo wa kuhifadhi nafaka kwa kujenga vihenge na maghala ya kisasa ili kuboresha miundo ya uhifadhi katika eneo la Makambako. Kukamilika kwa mradi huu kutawezesha kuongeza uwezo wa kuhifadhi nafaka kutoka tani 22,000 zilizopo sasa hadi tani 62,000.

Nafaka zinazonunuliwa, kuhifadhiwa na kuzungushwa/kuuzwa kupitia Kanda ya Makambako ni mahindi na mpunga. Kanda hii kijiografia huwa na uwiano mzuri wa uzalishaji wa mpunga na mahindi kutokana na kuwa na uzalishaji mkubwa wa ziada ya nafaka na imekuwa ni sehemu ya kivutio kwa wanunuzi mbalimbali wa nafaka kutokana na kupatikana kwa wingi na urahisi wa usafirishaji kwa njia ya reli na barabara.

Mawasiliano;