Habari

WAZIRI BASHUNGWA ATOA RAI KWA NFRA KUENDELEZA KASI YA UHIFADHI WA CHAKULA NCHINI

WAZIRI BASHUNGWA ATOA RAI KWA NFRA KUENDELEZA KASI YA UHIFADHI WA CHAKULA NCHINI
Aug, 13 2023

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Innocent Bashungwa ametembelea Banda la Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) lililopo katika maonesho ya Wakulima Nane Nane yanayofanyika Kitaifa Mkoani Mbeya.

Mhe. Waziri Bashungwa alipata wasaha mzuri wa kupatiwa maelezo mafupi na Mkurugenzi wa Masoko Bw. Mikalu Mapunda yanayohusu uhifadhi na kazi mbalimbali za Wakala.

Aidha, Waziri Bashungwa aliwapongeza NFRA kwa huduma zao wanazozitoa kwa wananchi kipindi cha ununuzi wa nafaka na mauzo ya mahindi kupunguza makali ya kupanda kwa bei za vyakula.

" Nijukumu kubwa sana mmepatiwa NFRA kuhakikisha Nchi yetu inakuwa na utoshelevu wa chakula na tunampongeza sana Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia mabilioni ya fedha yatakayo wawezesha kununua chakula cha kutosha nchini". Amesema Mhe. Waziri Bashungwa.