Habari

WANANCHI WAPONGEZA UTENDAJI WA NFRA KWENYE HUDUMA YA UUZAJI MAHINDI

WANANCHI WAPONGEZA UTENDAJI WA NFRA KWENYE HUDUMA YA UUZAJI MAHINDI
May, 31 2023

Wananchi wa Kata ya Chilonwa Wilayani Chamwino jijini Dodoma wameipongeza Serikali kupitia Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula NFRA kwa kufungua kituo cha mauzo ya mahindi, hivyo kuwezesha wananchi kupata huduma ya kununua Mahindi ya kupunguza makali ya kupnda kwa bei.

Wakazi hao wamesema hali yao kwa sasa ni ngumu hususan kipindi hiki ambacho bado mazao yapo mashambani hivyo Mahindi hayo yatawawezesha kupunguza makali ya upatikanaji wa Chakula Majumbani.

Kwa upande wake Shida Mapinga Mkulima na Mkazi wa Kijiji Cha Membe amesema wanafurahia huduma ya mauzo ya nafaka kwa bei nafuu ambayo inatolewa na NFRA kwa utaratibu mzuri.

"Japo watu ni wengi wanataka huduma hii lakini tunashukuru Kwa hiki tunachokipata hali ni mbaya mashambani hivyo tunawaomba NFRA waendelee kutuletea mahindi, wasisitishe mpaka tutakapoivisha mazao yetu shambani" amesema Shida