Habari

KATIBU TAWALA; KUSAYA APONGEZA JUHUDI ZA WAKALA KATIKA ZOEZI LA UNUNUZI WA NAFAKA MSIMU HUU

KATIBU TAWALA; KUSAYA APONGEZA JUHUDI ZA WAKALA KATIKA ZOEZI LA UNUNUZI WA NAFAKA MSIMU HUU
Jul, 24 2023

Wajumbe wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) wamekutana na Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa, Ndugu Gerald Kusaya na kufanya mazungumzo Kabla ya kuendelea na ziara yao Mkoni humo ambapo watatembelea ofisi za NFRA, Kanda ya Sumbawanga pamoja na vituo mbalimbali vya Ununuzi wa Mazao ya Nafaka (mahindi na mpunga).

Katika Mazungumzo hayo, Katibu Kusaya amepongeza sana Wakala hususani kwa juhudi zinazofanywa ikiwemo kutoa huduma za kuwauzia mahindi ya bei nafuu Wananchi kukabiliana na upungufu na makali ya bei za soko pamoja na kununua nafaka kutoka kwa Wakulima na Wafanya biashara ikiwahakikishia Watanzania soko la uhakika kwa kuwapatia bei nzuri.

Aidha, amewahakikishia kutoa ushirikiano wa hali na mali kufanikisha dhumuni la Taifa katika Uhifadhi wa Chakula na kuhakikisha Usalama wa Chakula Nchini linafikiwa.

"Ni jambo jema sana Wakala unalifanya na sisi kama Wana Rukwa, tunawahakikishia kuwa Chakula kipo na tutaendelea kuwahamasisha Wakulima walete nafaka vituo vya ununuzi. Pia, tunaona Wakala umetoa bei nzuri ya Mahindi, tunawapongeza sana sana" amesema Katibu Kusaya.