Habari

RAIS SAMIA AZINDUA MRADI WA KISASA WA KUHIFADHI NAFAKA

RAIS SAMIA AZINDUA MRADI WA KISASA WA KUHIFADHI NAFAKA
May, 31 2023

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, amezindua Mradi wa kuongeza uwezo wa kuhifadhi nafaka.


Uzinduzi huo umefanyika tarehe 22 Novemba, 2022 mkoani Manyara Wilaya ya Babati, Kata ya Maisaka Makatanini.

Aidha, mradi huo umehusisha Vihenge nane (8) vya kisasa, Maghala mawili (2), Ofisi za wafanyakazi, Sehemu ya Chakula (Canteen), Stoo ya kuwekea vitu, mzani wa kisasa wa kupimia Mazao pamoja na Maabara ya kisasa.

Mradi huo umekamilika kwa asilimia 100% na umeongeza uwezo wa Wakala wa kuhifadhi kutoka Tani 251,000 Hadi kufikia Tani 341,000.