NFRA imeendesha mafunzo kwa watumishi wake wa ubora ili kuwaongezea uwezo wa kudhibithi ubora wa chakula kinachohifadhiwa na Wakala.
Mafunzo hayo ya siku tatu yalifanyika kwenye ofisi za Makao Makuu ya Wakala jijini Dodoma yalilenga kuwajengea uwezo wafanyakazi wote wa ubora wa Wakala ili kuleta tija na ufanisi katika kazi hiyo ndani ya Wakala.