Habari

MENEJIMENTI YA NFRA YAKUTANA KUWEKA MIKAKATI YA KUBORESHA HUDUMA ZA WAKALA.

MENEJIMENTI YA NFRA YAKUTANA KUWEKA MIKAKATI YA KUBORESHA HUDUMA ZA WAKALA.
Sep, 11 2023

Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA), CPA Milton Lupa, amefungua Kikao cha Menejimenti ya Wakala tarehe 28 Agosti, 2023 Mkoani Morogoro.

Katika ufunguzi wa Kikao hicho Afisa Mtendaji Mkuu ambaye pia ni Mwenyekiti wa Menejimenti hiyo aliwashukuru Wajumbe hao kwa kuweza kuhudhulia kikao hicho ikiwa lengo kuendelea kujadili masuala mbalimbali ya kimkakati katika kuiendesha NFRA.

CPA Lupa alisisitiza kuendelea kwa ushirikiano baina ya Menejimenti na Watumishi wengine katika sehemu za kazi Ili kuleta umoja katika utekelezaji wa majukumu ya Wakala kwenye utoaji wa huduma za msingi Kwa jamii.

" Sisi ni kioo kama Viongozi ambao chini yetu kuna watu tunawaongoza na nafurahishwa sana na utendaji wenu hususani katika nafasi zenu za kazi lakini ni vyema kuweka ushirikiano baina yetu na Watumishi wengine ukizingatia NFRA ni Taasisi ya kimkakati" amesema CPA Lupa.