Habari

NFRA YAPATA WATUMISHI WAPYA 14 WA KADA MBALIMBALI

NFRA YAPATA WATUMISHI WAPYA 14 WA KADA MBALIMBALI
Oct, 23 2023

Meneja Rasilimali Watu wa Wakala wa Taifa ya Hifadhi ya Chakula (NFRA), Bw. Mulegi Majogoro, akizungumza na Wafanyakazi wapya wa. NFRA baada ya kupatiwa mafunzo maalumu ya utumishi wa Umma pamoja na maelezo mafupi kujua wajibu na majukumu ya NFRA Kabla hawajaenda kwenye Vituo vyao vya kazi.

Majogoro alisisitiza umuhimu wa Watumishi hao kuwa na umoja na ushirikiano katika kazi pia kuongeza bidii na kuheshimu Wakuu wao katika maeneo ya kazi watakayopangiwa.

Watumishi wapya 14 wamepangiwa vituo vya kazi katika kanda mbalimbali za Wakala.