Habari

NFRA YAKAMILISHA MKATABA WA MAUZO YA MAHINDI TANI 17,000 NCHINI ZIMBABWE

NFRA YAKAMILISHA MKATABA WA MAUZO YA MAHINDI TANI 17,000 NCHINI ZIMBABWE
Dec, 24 2019

Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya chakula uliingia mkataba wa kuuza tani 17,000 za mahindi na Serikali ya Zimbabwe tarehe 02 Septemba, 2019 Ilikubaliwa kuwa tani zote zitatoka kwenye kanda ya makambako kadhalika kanda hiyo ilipewa jukumu la kusimamia upakiaji wa mahindi kwenye mabehewa ya TAZARA tayari kwa kusafirisha kwenda Bulawayo Harare Zimbabwe.

Kanda ya makambako inavyo vituo vikuu viwili vya kuhifadhia ambavyo ni Makambako na Mbozi katika utekelezaji wa mkataba huo ilikubaliwatani 7,000 zichukuliwe kutoka kituo cha Makambako, na tani 10,000 kutoka kituo cha Mbozi.

Kazi rasmi ya kupakia kwenye behewa na kusafirishamahindikwenda Zimbabwe ilianza tarehe 17 Septemba, 2019 na ilianza kwenye kituo cha Makambako kwa kuwa TAZARA walikuwa wameandaa mabehewa tayari kwenye kituo hicho. Upakiaji kwenye kituo cha Mbozi ulianza tarehe 20 Septemba, 2019

Utekelezaji wa tani 7,000 kituo cha makambako ulimalizika tarehe 25oktoba, 2019 lakinikituo cha Mbozi ambacho kilipangiwa kutoa tani 10,000 kazi ilimalizika tarehe 26 Novemba, 2019.

Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya chakula (NFRA) umefanikiwa kutekeleza mkataba kwa asilimia 100, hadi kufikia tarehe 26.11.2019 ambapo kiasi cha tani 17,000 zilikuwa zimeshapakiwa nakukabidhiwa kwa wasimamizi wa mzigotayari kwenda Bulawayo Harare –Zimbabwe.


Muda wa kutekeleza mkataba ulikuwa ni siku 120 kuanzia tarehe 02.09.2019 hata hivyo Wakala umetekeleza kwa siku 86.


NFRA ilikuwa na uwezo wa kutekeleza mkataba huo ndani ya miezi miwili tu, kutokana na changamoto mbalimbali zilizojitokeza mkataba huo ulifikia siku 86.

Changamoto zilizojitokeza ni pamoja na Ucheleweshaji wa mabehewa, Uchache wa maturubai ya kufunikia mabehewa, na Hali ya hewa kubadilika mara kwa mara kutokana na msimu wa mvua.