Habari

WATUMISHI WANAWAKE WA NFRA KUSHIRIKI SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

WATUMISHI WANAWAKE WA NFRA KUSHIRIKI SIKU YA WANAWAKE DUNIANI
May, 31 2023

Watumishi Wanawake kutoka Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) wameungana na Wanawake wengine nchini kusherehekea Sikukuu ya Wanawake Duniani ambayo hufanyika Kila tarehe 8 mwezi Machi kila mwaka.

Sherehe hizo kimkoa zimefanyika Wilayani Kondoa Mkoani Dodoma ambapo Wanawake kutoka katika Taasisi mbalimbali za kiserikali na zisizo za Kiserikali wamekutana pamoja na kuadhimisha siku hiyo yenye kauli mbiu ya " Ubunifu na Mabadiliko ya Teknologia, Chachu Katika Usawa wa Kijinsia".