Habari

WAKULIMA WAFURAHISHWA NA BEI NZURI YA UUZAJI WA NAFAKA ZAO KWA NFRA

WAKULIMA WAFURAHISHWA NA BEI NZURI YA UUZAJI WA NAFAKA ZAO KWA NFRA
Jul, 24 2023

Baadhi ya wananchi wa Wilaya ya Ileje Mkoani Songwe wamefurahishwa na bei nzuri inayotumiwa na NFRA kununua nafaka katika Mkoa huo.

Wananchi hao wanasema hayo walipofikisha shehena zao za nafaka katika kituo cha ununuzi cha NFRA Isongole kilichopo Wilayani humo.

Wamesema Serikali kwa sasa imeamua kumnufaisha mkulima kwa kununua mazao kwa bei nzuri ambazo zinawafaidisha wakulima na kupata faida pindi wauzapo nafaka zao.

Sophia Mwaikomba ambaye ni Mkulima na Mkazi wa Kijiji cha Inyara amesema kwa sasa furaha yao kubwa kuona mabadiliko katika soko la nafaka nchini ambapo Serikali ya awamu ya sita ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imekuja kugeuza Kilimo kuwa cha kibiashara chenye kuleta tija kwa mkulima.

"Tulisikia kwenye vyombo vya habari Mhe. Waziri wa Kilimo akitaja bei elekezi za mazao mahindi na sisi tukashawishika kuleta mahindi yetu hapa NFRA na pia tunawashukuru sana NFRA kwa sasa tuna uwezo wa kuwaletea mazao yetu na mkatupa bei nzuri sana" amesema Sophia.