Habari

​Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) YAKUTANA MKOANI RUKWA

​Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) YAKUTANA MKOANI RUKWA
May, 31 2023

Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) imefanya Kikao tarehe 15 na 16 Desemba 2022 Mkoani Rukwa, katika Ukumbi wa mikutano wa NFRA-Kanondo, ikiwa Kikao cha kupitia utekelezaji wa majukumu ya Wakala kufikia mwezi Novemba, 2022.

Kikao hicho kiliongozwa na Kaimu Mwenyekiti Ndugu Elimpaa Kiranga.

Bodi hiyo pia ilitembelea eneo la Mradi wa Kuongeza Uwezo wa Kuhifadhi Nafaka ambao umekamilika na kukabidhiwa kwa NFRA hivi karibuni.