Afisa Mtendaji Mkuu Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA), CPA Milton Lupa, amefanya ziara katika vituo vya mauzo ya Mahindi vilivyopo Kanda ya Dodoma katika Wilaya ya Dodoma Mjini, Chamwino pamoja na Mpwapwa.
CPA Lupa amefanya ziara hiyo na kufurahishwa na huduma zinazoendelea kutolewa na Watumishi wa NFRA pia amefurahi kuona wingi wa watu wakipata huduma hiyo bila adha yoyote.
Aidha, amewahakikishia wananchi kuwa NFRA ina Chakula Cha kutosha hivyo watatoa huduma hiyo mpaka pale watakapo ona Hali ya upungufu wa Chakula inatoweka.
Amesema Kwa sasa NFRA inahudumia vituo zaidi ya 170 nchi nzima hivyo wanafanya juhudi ya kusogeza Mahindi kutoka katika Kanda mbalimbali Ili wananchi waendelee kupata huduma hiyo ya Mahindi ya bei nafuu.
" Tutafanya kadri iwezavyo kuhakikisha mnapata mahindi ya kutosha na sisi kama tulivyo agizwa na Kiongozi wetu tutaweza kuwahudumia mpaka pale mtakapo ivisha Chakula chenu mashambani" amesema CPA Lupa.
NFRA inaendelea na zoezi la uuzaji wa mahindi kwa bei nafuu ambapo wananchi wameendelea kutoa shukrani zao kwa NFRA na kupongeza juhudi zinazofanywa na Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan kuwapatia huduma hiyo kwa lengo la kupunguza makali ya bei za vyakula.