Mkuu wa kitengo cha usafirishaji Mpango wa Chakula Duniani (WFP) Ndg Mahamood Mabuyu amesema kuwa WFP imeanza kusafirisha mahindi iliyoyanunua kwa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula NFRA kupeleka nchini Uganda.
Alisema WFP imenunua Tani 36,000 za mahindi kwa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) ambapo mkataba wa mauziano ulisainiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli tarehe 4 Januari 2019
Alisemaa WFP inanunua mahindi nchini Tanzania yenye thamani ya Bilioni 21 kutoka NFRA.
Alisema WFP imekwishanunua Tani 136,000 za mahindi Tangu Julai mwaka 2018 na kati ya hizo Tani 36,000 ni fursa zilizoibuliwa na WFP za mtama zinazohitajika Sudani ya Kusini.
Katika hatua nyingine Ndg Mabuyu amemshukuru Rais wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli kwa ushirikiano anaoutoa katika utekelezaji wa mradi huo kupitia taasisi mbalimbali ambazo ni NFRA, TRA, Shirika la Reli, TBS na nyinginezo.
Alisema taasisi hizo zimekuwa na ushirikiano mwema katika kuhakikisha ubora unasimamiwa ipasavyo.