Habari

HAYA NDIYO MAJUKUMU YETU SISI KAMA WAKALA LAZIMA TUFIKIE MALENGO

HAYA NDIYO MAJUKUMU YETU SISI KAMA WAKALA LAZIMA TUFIKIE MALENGO
Nov, 09 2023

Afisa Mtendaji Mkuu mpya wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula NFRA Dkt Andrew Komba, amefanya kikao cha kwanza na Menejimenti ya Wakala ya Wakala ya Makao Makuu na Kanda.

Kikao hicho kilifanyika Makao Makuu ya NFRA Jijini Dodoma na kuhudhuriwa na Maneneja wa Kanda za Wakala, Wakuu wa Vitengo na Wakurugenzi wa Idara.

Dkt. Komba alisisitiza ushirikiano katika kazi mbali na kutimiza vyema majukumu ya Wakala katika utoaji huduma za msingi kwa jamii na kutengeneza misingi ya Wakala kujiendesha kibiashara.

"Sisi Kwa umoja wetu tuna “mandate” ya kuhakikisha tunakuza Biashara yetu ya nafaka tukumbuke kuwa kwa sasa Serikali na umma unatutazama katika kujiimarisha kwenye kuongeza uwezo wa kuhifadhi nafaka uhifadhi mkubwa na kupanua wigo wa utoaji wa huduma zetu za ununuzi na uuzaji wa nafaka". amesema Dkt. Komba