Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) wametangaza rasmi kuanza kununua mazao ya wakulima kupitia vituo vyake vilivyopo katika maeneo mbalimbali nchini.
Akizungumza wakati wa mahojiano kwa njia ya runinga katika kipindi cha Jambo Tanzania, Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA), CPA Milton Lupa, amesema ununuzi huo utaanza katika maeneo ambayo tayari Wakala umejiridhisha kwamba mazao yameanza kukauka. Aidha, ilibainishwa kwamba kwa sasa NFRA itanunua mahindi na mpunga kupitia utaratibu wa kufungua vituo vya ununuzi ambavyo Wakulima watauza mahindi yao na kutumia Vikundi vya wakulima/Ushirika na Mawakala/Wafanyabiashara.
“Kwa sasa tumeishaanza kununua mazao baadhi ya maeneo kwa kufungua vituo vyetu na tutaendelea kufungua vituo zaidi, hivyo nitoe wito kwa wakulima kutumia fursa ya bei nzuri kuleta kuuza mazao zaidi” amesema CPA Lupa