Habari

NFRA YASHINDA TUZO SIKU YA MBOLEA DUNIANI

NFRA YASHINDA TUZO SIKU YA MBOLEA DUNIANI
Oct, 23 2023

Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) wamekabidhiwa tuzo ya uoneshaji bora katika maonesho ya siku ya mbolea Duniania ambayo kitaifa kwa mwaka huu yamefanyika Mkoani Tabora.

Tuzo hiyo wamekabidhiwa na Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. David Silinde ambapo aliwapongeza sana kwa hatua hiyo na kuwataka kuendelea kuongeza bidii hususani katika maonesho mbalimbali ya kitaifa lengo kuhakikisha elimu inawafikia wananchi.