Habari

TUNATAKA NFRA IWE MKOMBOZI WA TANZANIA NA NCHI ZA KARIBU KATIKA UHIFADHI

TUNATAKA NFRA IWE MKOMBOZI WA TANZANIA NA NCHI ZA KARIBU KATIKA UHIFADHI
Nov, 09 2023

Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA), Dkt. Andrew Komba, amefanya kikao cha kwanza na Wafanyakazi wa Wakala Makao Makuu pamoja na Kanda ya Dodoma.

Kikao hicho kimefanyika Leo Tarehe 03/10/2023 katika ofisi za Makao Makuu ya NFRA Jijini Dodoma.

Katika Kikao Dkt. Komba aliwasisitizia zaidi Wafanyakazi hao kushirikiana kwa umoja katika kutimiza majukumu ya Wakala hususani kutoa huduma Kwa jamii kama ilivyo wajibu wake.

Aidha alieleza kuwa Wakala Kwa Sasa unamkakati mkubwa wa kuongeza tija ya uhifadhi Chakula mpaka kufikia Tani laki 4 Ili kuiwezesha Taifa katika upatikanaji wa Chakula nchini.

" Tunataka Taasisi hii iweze kuwa na uwezo mkubwa wa kuhifadhi chakula cha kutosha na inapoitoa inakwenda kubadilisha soko la mazao Tanzania na Nchi jirani hivyo nguvu ya kufanikisha hili ni sisi kushirikiana kwa pamoja" amesema Dkt. Komba.