Habari

KAMATI YA PAC YAKAGUA UJENZI WA MRADI WA KUONGEZA UWEZO WA KUHIFADHI NAFAKA UNAOJENGWA NA NFRA

KAMATI YA PAC YAKAGUA UJENZI WA MRADI WA KUONGEZA UWEZO WA KUHIFADHI NAFAKA UNAOJENGWA NA NFRA
Jan, 15 2020

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) tarehe 14 januari 2020 imetembelea Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Makao Makuu eneo la Kizota Viwandani Jijini Dodoma.

Kamati hiyo ikiongozwa na makamu mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe Aeshi Khalfan Hilaly ambaye ni mbunge wa jimbo la Sumbawanga mjini mkoani Rukwa imerishishwa na mpango huo wa Serikali katika kukabiliana na uwezo mdogo wa kuhifadhi nafaka.

Katika ukaguzi huo kamati hiyo imepokelewa na mwenyeji wake ambaye ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula Ndg. Milton Lupa akiwa ameambatana na timu nzima ya menejimenti ya (NFRA)

Kadhalika akiongea baada ya kukagua mradi huo mwenyekiti wa Kamati ya Bunge alisifu mradi na kusema ni moja kati ya miradi yenye tija kwa maendeleo ya nchi kwani mara baada ya mradi huo kukamilika uwezo wa kuhifadhi Wakala wa Taifa utakuwa mara mbili ya uwezo wa sasa yaani kutoka kutoka tani 251000 hadi tani 501000 huku ikitarajiwa kufikia tani 700000 kufikia mwaka 2025

Mikataba ya mradi wa kuongeza uwezo wa kuhifadhi chakula ilisainiwa na kuanza kazi tarehe 09 Desemba 2017 kati ya nfra na makampuni mawili toka Poland ambayo ni Feerum S.A na Unia spzo.o. Aidha mradi huo utatekelezwa kwa gharama ya dola za Kimarekani milioni 55 na unatarajiwa kukamilika ndani ya kipindi cha miezi kumi na nane (18) kuanzia mwezi mei 2018.

Aidha Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula unamiliki maghala ya kuhifadhi nafaka 34 yenye uwezo wa kuhifadhi jumla ya tani 251,000 uwezo huu wa sasa wa maghala hautoshelezi mahitaji ya dharula ya chakula kwa mfulullizo wa miezi mitatu (3) kwa akiba isiyopungua tani 700,000 hivyo kupelekea uhitaji wa kuongeza uwezo wa uhifadhi.