Habari

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe Afunga kikao cha Bodi ya Ushauri ya NFRA

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe Afunga kikao cha Bodi ya Ushauri ya NFRA
May, 21 2021

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe, Amefunga kikao cha Bodi ya ushauri ya NFRA huku akisisitiza utafutaji wa Masoko ya mazao ya wakulima ndani na nje ya nchi.

Naibu Waziri aliitaka NFRA kutafuta masoko ya mazao ya wananchi hususani mahindi nje nchi na ikiwezekana kukodi maghala kwenye mipaka kama vile Sudan Kusini na Uganda ili kurahisisha upatikanaji wa masoko ya nje ya nchi.